The House of Favourite Newspapers

MAMA’KE MKUBWA DIAMOND ALILIA TALAKA BAKWATA

Shani Swedi.

 

DAR ES SALAAM: Wakati mama yake mzazi Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ akila bata na mumewe ambaye amemzidi umri (dogodogo), mama yake mkubwa staa huyo, Shani Swedi yeye amekwenda Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kudai talaka yake kwa mwanaume ambaye pia amemzidi umri (dogodogo) aliyefahamika kwa jina la Ajazi.

 

UBUYU WA AWALI

Awali, Amani lilipenyezewa ubuyu kuwa, Shani ambaye ni dada yake na mama Diamond, ametinga Bakwata, mtaa wa Lumumba na Aggrey, Kariakoo jijini Dar kudai talaka hiyo baada ya kuchoshwa na upweke wa bwana wake huyo aliyemuoa miaka kadhaa iliyopita.

Shani Swedi na Mama Diamond.

 

“Amekuja hapa mama’ke Rommy kudai talaka, amesema amechoka sana kwani mumewe huyo amebadilika sana baada ya kumuoa mke mwingine mdogo mdogo wanayeendana umri. Yeye ukimuangalia ni mkubwa sana kwa huyo mumewe. Bakwata wao bila hiyana wamempa barua ya kumuita mumewe ili aje wazungumze na ikiwezekana atoe talaka hapahapa,” Amani lilielezwa.

AMANI LANASA BARUA

Kama hiyo haitoshi, Amani lilifanikiwa kuinasa barua ya wito wa kumuita Ajazi Februari 27, mwaka huu shaurini ambayo ilikuwa rasmi ikiwa na mhuri wa Bakwata.

Shani Swedi akiwa na mwanaye Rommy Jones.

 

HAWAKUTOKEA

Kwa mujibu wa mtu aliye karibu na ofisi za Bakwata, siku Ajazi aliyoitwa shaurini hakutokea na badala yake, ilielezwa kuwa alimuita mama Rommy kazini kwake ili waweze kuzungumza.

“Jamaa hakutokea ila nasikia ilibidi amuite kazini kwake, wakazungumza lakini hata hivyo hawakufikia muafaka wa talaka.

“Inavyoonekana, mume anakuwa mzito kutoa talaka licha ya kuwa wana muda mrefu hawajakutana kimwili lakini mke amechoka maana anaona hakuna sababu ya kuwa na kipingamizi, anataka talaka yake,” alidai mtu huyo.

Ajazi na mke mdogo.

 

MAMA ROMMY AFUNGUKA

Ili kuupata ubuyu kamili, Amani lilimvutia waya mama yake Rommy ili kuweza kumsikia anazungumziaje sakata hilo ambapo bila hiyana alimwaga ubuyu kamili.

CHANZO CHA KUSHANGAZA

“Ni kweli, nimekwenda Bakwata kudai talaka sababu amenitelekeza kwa muda mrefu na hata kihuduma.

Ajazi na mama Diamond.

 

KUHUSU KUMZIDI UMRI

“Mume wangu ni kweli nimempita miaka mingi kiumri, kama miaka kumi na mbili hivi. Kila nikimwambia kuhusu habari ya talaka ananizungusha.

“Mara ya mwisho nilienda kwake akanizungusha. Kuna wakati nilimpa karatasi ili aweze kuandika. Akasema hajui. Ikashindikana.

 

ATINGA OFISINI KWAKE

“Hivi juzijuzi nilienda ofisini kwake, akaniahidi Jumamosi (iliyopita) niende nyumbani kwake nikachukue.

“Sasa mimi nilishindwa kwenda sababu nilishangaa ametaka niende nyumbani kwake ghafla wakati siku zote alikuwa hataki niende,” alidai mama Rommy na kuongeza:

“Kimsingi hapa katikati nilikuwa nimelazwa naumwa. Lakini mimi sasa hivi ninachotaka ni talaka yangu tu na hata mkimpigia yeye mwambieni hivyo mimi nataka talaka yangu.”

Mke mdogo.

 

HANA KINYONGO?

Akizidi kushusha ubuyu, bi mkubwa huyo alisema, kwa upande wake hakuwa na kinyongo chochote na mumewe lakini kwa kuwa aliamua kuoa mke mwingine na kumtelekeza yeye muda mrefu bila kumpa huduma, basi ampe talaka yake.

“Si kwamba nimedai talaka kwa sababu nina wivu au nini, hapana! Kimsingi dini yetu ya Kiislamu inaruhusu mwanaume kuoa hata wanawake watatu lakini yeye hakunipa heshima yangu kama mke mkubwa. Aliamua kuoa bila hata mimi kujua, sasa mimi ninachohitaji ni talaka tu niwe huru,” alisema mama Rommy.

Alipoulizwa kama mumewe huyo labda anaendana umri na mwanaye Rommy, bila kutaja umri wao, alisema si kweli kwani mumewe huyo ni mkubwa kuliko mwanaye Rommy.

Mama Diamond na mumewe.

HUYU HAPA AJAZI

Amani lilimpomvutia waya Ajazi ili kumsikia kwa nini anasita kutoa talaka, alisema kwa upande wake ameshaachana na mwanamke huyo miaka mitatu iliyopita.

“Kwa sheria ya dini yetu, ukikaa hata miezi sita tu bila mkeo, si mkeo,” alisema Ajazi.

 

SARESARE

Mama Diamond na mama Rommy ambao ni mtu na dada yake, inaonekana kwa pamoja wana bahati ya kuanguka kwenye penzi na vijana waliowazidi umri (dogodogo) kwani awali alifahamika mama Diamond, sasa dada yake naye kumbe aliolewa na ‘Serengeti boy’.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

 

 

Mama A’ke Mkubwa Diamond! Alilia Talaka Bakwata

Comments are closed.