The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mambo ya Kuepuka Kwa Wagonjwa wa Kisukari kwa Udhibiti Bora wa Sukari

0


Ingawa vyakula vingine vinaweza kusaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari, vingine vinaweza kuharibu usawa wa sukari ya damu na kuongeza hatari ya matatizo. Kuzuia au kuepuka yafuatayo kunaweza kusaidia udhibiti bora wa glukosi mwilini na afya kwa ujumla ya mtu.

Vinywaji vya Sukari na Pipi
Vinywaji kama vile soda, juisi zilizotiwa sukari, vinywaji vya kuongeza nguvu (energy) au zilizotengenezwa kwa sukari iliyosafishwa kiwandani husababisha kuongezeka kwa kasi kwa sukari kwenye damu kwa mtu mwenye kisukari. Pia huongeza kalori tupu bila thamani ya lishe, na kuchangia kupata uzito na kupata upinzani wa insulini inayothibiti sukari kwenye damu.

Nafaka Iliyosafishwa na Mkate Mweupe
Mchele mweupe, keki, ice cream, mkate mweupe na bidhaa zingine za nafaka zilizosafishwa au kukobolewa hukosa nyuzinyuzi na kuyeyushwa haraka, na kusababisha kuongezeka kwa ghafla kwa viwango vya sukari kwenye damu.
Kukoboa nafaka na kuzibadilisha nafaka nzima hutoa virutubisho vinavyotakiwa mwilini na huondoa udhibiti bora wa glukosi kwenye damu kwa mgonjwa wa kisukari.

Vyakula vya Kukaanga na Kusindikwa
Vyakula vya kukaanga kama chipsi, ndizi mbivu, mihogo mara nyingi huwa na mafuta yasiyofaa kwa mgonjwa wa kisukari na huwa na sodiamu na kalori nyingi. Nyama iliyochakatwa kiwandani na vyakula vilivyo tayari kuliwa vilivyopitia kiwandani vinaweza pia kuchangia kuongezeka kwa sukari mwilini na mgonjwa kuwa na afya duni ya kimetaboliki.

Maziwa Yenye Mafuta Kamili na Mafuta Yaliyojaa
Maziwa yote, cream, siagi na jibini iliyojaa mafuta yana kiasi kikubwa cha mafuta yaliyojaa ambayo yanaweza kuongeza viwango vya cholesterol na hatari ya ugonjwa wa moyo kwa wagonjwa wa kisukari. Kuchagua kula vyakula vyenye mafuta ya mimea au mbogamboga kwa ujumla ni chaguo bora zaidi kwa mtu mwenye kisukari.

Mapishi Yanayofaa Kisukari
Anza siku yako ya asubuhi kwa bakuli la uji wa moto wa ulezi au uwele wenye karanga iliyosagwa. Mlo huu husaidia kuweka viwango vyako vya nishati sawa.

Chakula cha mchana
Weka pamoja saladi na mboga za majani, nyanya, tango, parachichi iliyokatwa na kuku aliyekaushwa kwa mafuta ya mzeituni na maji ya limao kwa ladha ya ziada. Kula na ugali wa uwele au ulezi.

Chakula cha jioni
Viazi vitamu vilivyochomwa na brokoli iliyokaushwa inafaa kwa chakula cha jioni. Mlo huu hukupa protini yenye afya, wanga kidogo na nyuzinyuzi nyingi zifaazo mwilini.

Unaweza kula vipande vya apple na siagi ya almond au karanga zilizochanganywa, zinafaa kwako! Kiganja kidogo cha karanga zilizochanganywa, Yoghuti iliyotiwa juu na kunyunyizia mbegu za chia, Mboga safi kama vile vijiti vya karoti au pilipili hoho humfaa mwenye kisukari.

Makala na Elvan Stambuli | GPL.

SAKATA la KUTOWEKA kwa POLEPOLE – RC CHALAMILA AVUNJA UKIMYA – AWATAKA WANANCHI WAAMINI POLISI..


 

Leave A Reply