The House of Favourite Newspapers

Man City Haikamatiki, Yaipiga Tottenham Hotspur Mabao 4-1

Kevin De Bruyne katikati akishangilia na wenzake.

NI kama haina mpinzani katika Ligi Kuu ya England kwani Manchester City jana usiku iliifunga Tottenham Hotspur mabao 4-1 na kujiimarisha kileleni mwa Premier League.

 

Ushindi huo umeifanya Man City inayonolewa na Pep Guardiola kufikisha pointi 52 huku anayefuatia Manchester United akiwa na pointi 38. Man United leo inacheza na West Brom katika ligi hiyo. Spurs imebaki na pointi 31 na imeshuka hadi naafsi ya saba.

Mabao ya Man City yalifungwa na Ilkay Guendogan dakika ya 14 baada ya kupokea pasi ya Leroy Sane huku bao la pili likifungwa na Kevin De Bruyne akimalizia pasi ya Guendogan. Bao la tatu lilifungwa na Raheem Sterling dakika ya 80, Sterling alifunga bao la nne dakika ya 90. Spurs ilipata bao lake dakika ya 90 mfungaji akiwa ni Christian Erikssen

Gabriel Jesus akijiandaa kuingia Uwanjani.

Man City imeendeleza rekodi ya kutofungwa msimu huu kwani hadi sasa imecheza mechi 18 ambapo imeshinda mara 17 na kutoka sare mara moja.

MSIMAMO TOP FIVE PREMIER

P W D L Pts

1.Man City 18 17 1 0 52

2.Man United 17 12 2 3 38

3.Chelsea 18 12 2 4 38

4.Arsenal 18 10 3 5 33

5.Burnley 18 9 5 4 32

Comments are closed.