The House of Favourite Newspapers

Man Fongo Kutambulisha Mpya Pasaka Dar Live

HITMAKER wa Ngoma ya Hainaga Ushemeji, Man Fongo anatarajia kutambulisha ‘dude’ jipya Aprili Mosi (Sikukuu ya Pasaka) katika Usiku wa Mwisho wa Ubishi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Man Fongo alisema kuwa, siku hiyo kwa mara ya kwanza mashabiki watapata kumsikia akiibuka na dude jipya ambalo limekaa mkao wa amshaamsha mwanzo mwisho (jina kapuni kwa sasa).

 

“Najua wajanja wote lazima waje Dar Live na pia lazima wamkute Man Fongo wa kitofauti, njoo washtue na wengine kwani siku hiyo nitawaonesha Singeli inaimbwaje na inachezwaje huku nikizindua ngoma mpya ambayo nikiitaja sasa nitakuwa naharibu njoo ushuhudie,” alisema Man Fongo anayebamba pia na ngoma kibao ikiwemo Nani Asiyependa na Safi Tu.

 

Mratibu na Meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP Mjomba’ aliongelea usiku huo kuwa, mbali na uwepo wa Man Fongo, jukwaa pia litawaka kwa burudani kutoka kwa mkali mwingine asiyeshikika kwenye Muziki wa Singeli, Sholo Mwamba.

“Hakuna mpenda Singeli asiyetambua shoo za Sholo Mwamba zinakuwaje. Katika Sikukuu ya Pasaka, Sholo ataliamsha kwa ngoma zake zote kali kuanzia Ronaldo, Ukinipa Sisemi pamoja na Ghetto,” alisema KP.

 

Katika shoo hiyo pia atakuwepo mkali mwingine wa muziki huo, Dulla Makabila ambapo atatoa sapraiz ya aina yake kwa kupanda na mwandani wake, Tiko Hassan na kuimba pamoja Singeli.

“Singeli itakuwa imeteka ukumbi mzima, Dar yote itahamia Dar Live kwa saa kadhaa. Dulla Makabila atahakikisha kila shabiki anacheza na kuimba naye pamoja nyimbo zake zote kuanzia Haujaulamba ‘Utatoa Hutoi’, Demu Wako Namba Ngapi pamoja na Makabila,” alisema KP.

 

KP aliongeza mbali na uwepo wa wakali wa Singeli, kuonesha kuwa utakuwa Usiku wa Mwisho wa Ubishi, katika Muziki wa Taarab napo kutakuwa na makundi yanayotikisa kama vile Yah TMK pamoja na Jahazi Modern.

“Wale wapenda Muziki wa Pwani nayo hii si ya kukosa, Yah TMK itakuwepo jukwaani kuoneshana umwamba na Jahazi Modern na niwaambie tu, burudani hii ya mwambao itaanza saa mbili za usiku kisha itafuatiwa na burudani ya Singeli.”

 

Kiingilio katika shoo hiyo ya aina yake kitakuwa ni buku s aba yaani shilingi 7,000 huku michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo kuogelea itafanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi 12 jioni kwa mtonyo wa buku tatu yaani shilingi 3,000.

SHOWBIZ XTRA

Comments are closed.