The House of Favourite Newspapers

Maua Sama Atamani Kuimba Gospo

Maua Sama

HITMAKER wa Ngoma ya Mahaba Niue, Maua Sama amefunguka kati ya vitu anavyotamani kwenye muziki kwa sasa ni kujiingiza katika Muziki wa Injili ‘Gospo’.

 

Akichonga na Showbiz Xtra, Maua anayebamba na Ngoma ya Nakuelewa alisema kuwa, japokuwa ni Muislam lakini amejikuta akitamani siku moja kuimba Injili.

 

“Napenda sana nyimbo za inspiration, kuna wakati nafikiria najikuta nikitamani kuimba hasa hizi za Gospo. Ipo siku nitaimba kwa sababu ni kitu ninacho-kipenda na kukitamani kutoka moyoni,” alisema Maua.

ANDREW CARLOS

Comments are closed.