The House of Favourite Newspapers

Man United na Barcelona Wafikia Makubaliano ya Usajili wa Kiungo wa Uholanzi

0
Kiungo wa FC Barcelona Frenkie De Jong

KLABU ya Manchester United ya Uingereza pamoja na FC Barcelona ya nchini Hispania wamefikia makubaliano ya uhamisho wa kiungo Frenkie De Jong raia wa Uholanzi anayekipiga katika klabu ya Barcelona kwa ada ya jumla ya Euro milioni 65.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Skysports ni kwamba mazungumzo bado yanaendelea kuangalia namna ya vipengele vya mkataba huo ili kuhakikisha dili hilo linakamilika kwa wakati.

 

Makubaliano binafsi kati ya mchezaji na Manchester United yanasemekana kuwa si tatizo.

De Jong akiwa na uzi wa Ajax kabla ya kutimkia Barcelona

De Jong amefanikiwa kucheza michezo 46 akiwa na uzi wa Barcelona msimu uliopita huku akiwa na jumla ya miaka minne iliyobakia kwenye mkataba wake wa sasa.

 

Ikumbukwe De Jong (25) alicheza chini ya Kocha wa sasa wa Manchester United Erik Ten Hag akiwa na klabu ya Ajax ambayo ilifanikiwa kuchukua Kombe la Eredivisie mara mbili mfululizo pamoja na kufanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Kocha Mpya wa Manchester United Erik Ten Hag

Ripoti za mwanzoni mwa mwezi huu zinadai kuwa usajili wa Frenkie De Jong ulikuwa ndiyo kipaumbele kwa kocha mpya wa Manchester United katika kufanya mabadiliko ya kikosi chake kuelekea msimu wa 2022/2023.

 

 

 

Leave A Reply