The House of Favourite Newspapers

MAPENDEKEZO YA BAJETI YA SERIKALI MWAKA 2018/19

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango.

1.0 UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa Hoja kwamba, Bunge lako sasa lipokee na kujadili mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2017/18 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka ujao wa fedha 2018/19.

 

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/19.

 

3. Mheshimiwa Spika, napenda nitumie fursa hii kuwapongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Taifa letu kwa ujasiri na uzalendo wa hali ya juu.

BONYEZA HAPA KUENDELEA KUISOMA

Comments are closed.