The House of Favourite Newspapers

Mashabiki United Wazoa Jezi Orijino Spoti Xtra

KATIKA jezi tatu orijino zilizotolewa jana kwenye droo ya shindano la Spoti Xtra, mbili zimekwenda kwa mashabiki wa Manchester United na moja kwa Liverpool.

Washindi hao walipatikana kwenye droo iliyochezwa jana saa 10:00 jioni kupitia kipindi maarufu cha michezo cha SPOTI HAUSI cha Global TV online.

 

Abel Antony wa Mlandizi, Kibaha na Geofrey Mohamed wa Bukoba ndio walioshinda jezi za Man United huku Nassor Gallu wa Temeke akiibuka na uzi wa Liverpool.

Katika droo ya jana, Venance Mwanga wa Muheza, Tanga ndiye aliyeibuka na zawadi kubwa ya Headphone orijino za Beats by Dre kutoka Marekani.

 

Washindi hao watakabidhiwa zawadi zao Jumatatu mchana kwenye ofisi za Spoti Xtra zilizoko Sinza Mori kwenye jengo la Global Group. Kwa mujibu wa uongozi wa Spoti Xtra zawadi kibao orijino zipo na wasomaji waendelee kushiriki kwenye droo hiyo kila Jumapili gazeti linapotoka.

 

Ili kushuhudia jinsi shoo ya jana ilivyochezeshwa chukua simu janja yako ingia kwenye mtandao wa Youtube tafuta SPOTI HAUSI ya Global TV Online.

AU TAZAMA HAPA

Comments are closed.