The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Wampa ‘Stress’ Mwasiti

MWANAMUZIKI Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’ aliyewahi kutikisa na ngoma kali ikiwemo Hao na Nalivua Pendo, amepenyeza kuwa kwa sasa mashabiki wamempa stress za kutaka kutoa wimbo kwa hiyo yupo chimbo akijipanga kurejea kwenye gemu kama ilivyokuwa zamani.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Mwasiti alisema kuwa kinachomfanya mpaka sasa awe bado ‘amesizi’ ni kwamba anaumiza kichwa kazi ya namna gani ambayo ataitoa na kukata kiu ya mashabiki wake kutokana na kukaa kimya muda mrefu.

“Unajua mashabiki wananipa stress kazi gani nitoe. Lakini niwaambie tu nitarudi kwenye gemu kama kimbunga. Nipo chimbo na muda wowote nikishakuwa na maamuzi sahihi ya kazi ipi nitoe mashabiki wangu watanisikia,” alisema Mwasiti.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA

Comments are closed.