testiingg
The House of Favourite Newspapers

Samatta Apewa Unahodha Genk

MAMBO yanazidi kumnyookea straika Mtanzania Mbwana Samatta katika kikosi cha KRC Genk baada ya Jumamosi iliyopita kuwa nahodha kwenye mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji walipocheza dhidi ya K.V. Oostende.

 

Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, alikuwa nahodha wa Genk kwenye mechi hiyo ambayo walishinda kwa mabao 3-1 kufuatia nahodha mkuu wa timu hiyo, Sébastien Dewaest kutokuwepo kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Luminus nyumbani kwa Genk.

 

Ushindi huo walioupata, umewafanya Genk kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi nane wakiwa kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo. Genk ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wapo nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara Standard Liege ambao wana pointi 15 kutokana na kucheza mechi saba.

Comments are closed.