The House of Favourite Newspapers

MASTAA HAWA WALIVYOTAMBA NA NEMBO ZA DINI


JUMAPILI iliyopita gumzo kubwa katika sekta ya burudani ilikuwa ndani ya Usiku wa Met Gala ambapo mastaa kibao wakiwemo Kim Kardashian, Lana De Ray Rita Ora, Rihanna, Anna Wintour, Jennifer Lopez na wengineo walitamba wakiwa katika mavazi yenye alama mbalimbali za Dini ya Kikristo.

Katika usiku huo wa Met Gala ambao zamani ulikuwa ukitambulika kama Met Ball lengo likiwa ni kuwakusanya mastaa karibu na kuonesha mavazi yao na kiasi kinachopatikana kuchangia Tasisi ya Makumbusho ya Sanaa ya Metropolitan, Rihanna alifunika kwa vazi lake lililobuniwa kwa shanga kubwa nyeupe huku kichwani akivalia kofia zinazotumiwa na viongozi wa dini ya kikristo.

Mastaa wengine waliovalia mavazi yenye nembo ya dini ni Kim Kardashian aliyevaa gauni la rangi ya dhahabu likiwa na nembo ya misalaba miwili eneo la tumboni na kiunoni, Katy Perry aliingia akiwa na vazi la mabawa mithili ya malaika, Jennifer Lopez alikuwa amevaa gauni refu jeusi lililochanganyika na kijani huku eneo la kifuani likuwa na msalaba mkubwa wa bluu na nyekundu.Jared Leto aliwashangaza wengi baada ya kuingia akiwa na muonekano unaofanania na Yesu huku kichwani akizungusha nakshinakshiza

 

Image result for Jennifer Lopez met gala 2018

NEW YORK, Marekani

Comments are closed.