The House of Favourite Newspapers

Matola: Simba bingwa Ligi Kuu Bara

KOCHA Mkuu wa Lipuli, Selemani Matola, amefunguka kuwa mpaka sasa ligi ilipofi kia, Simba ina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa kutokana na matokeo ambayo wamekuwa wakipata hivi karibuni.

 

Msimu uliopita, Simba ndiyo walikuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara na hadi sasa wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 66 tofauti ya alama nane dhidi ya Yanga mabao ndiyo vinara kwa pointi 74, lakini Simba wana viporo sita.

 

Wakishinda vitatu tu wanakaa juu ya Yanga. Akizungumza na Championi Jumamosi, Matola alisema Simba ina nafasi ya kutetea ubingwa kutokana na matokeo ambayo wamekuwa wakipata.

“Simba bado ninaiona ina nafasi kubwa msimu huu kuweza kutetea taji lao kutokana na aina ya matokeo ambayo wanapata sasa hivi na ukiangalia bado wana gepu kubwa na Yanga hivyo nafasi wanayo.

 

“Na hii ni kama watachanga vyema karata zao kwenye mechi zao ambazo zimesalia, ni nyingi tofauti na wapinzani wao Yanga ambao wamesaliwa na mechi sita tu kumaliza ligi.

 

“Japo wanacheza mechi mfululizo lakini wamekuwa wakipambana kibishi na kupata matokeo hivyo nafasi iko kwao japo wakati mwingine mpira unakuwa hautabiriki,” alisema Matola.

 

Matola kwa sasa timu yake inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na Mei 6, mwaka huu itavaana na Yanga katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Comments are closed.