The House of Favourite Newspapers

Maua Sama Ataja Mwaka wa Kuolewa

Maua Sama.

 

MKALI mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Maua Sama kwa mara ya kwanza ametaja mwaka wa kuolewa kuwa mambo yakienda sawa mwaka huu unaweza kuwa wake.

 

Awali zilienea tetesi kuwa, staa huyo anayebamba na Ngoma ya Nakuelewa amechumbiwa na mpenzi wake ambaye ni Mzungu lakini mwenyewe ameibuka na kukanusha.

 

“Nilishangaa kwa kweli hilo suala la kuchumbiwa na Mzungu kwani halikuwa la kweli, kuhusu kuolewa nimekuwa nikisikia kwa mashabiki sana, ndoa ni mipango, maombi yao yanaweza kunifanya nikatimiza hilo na inawezekana hata mwaka usiishe,” alisema Maua.

STAR SHOWBIZ

Comments are closed.