The House of Favourite Newspapers

MAUA SAMA : NAKUJA NA NAFUNGA JUMLA JUMLA

Maua Sama

BAADA ya wakali wa Hip Hop, Roma Mkatoliki na Stamina wanaounda Kundi la Rostam kuja na msemo wa Kufunga Jumla Jumla, mkali wa R&B Bongo, Maua Sama naye ameunga mkono msemo huo.  Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Maua Sama anayetamba na Ngoma ya Iokote alisema kuwa, ametokea kuvutiwa na msemo huo baada ya kuusikia na kwamba anatamani kuja na wimbo wenye jina hilo.

“Nimependa kwa kweli, kwa sababu msemo kama huu kutumika mwishoni mwa mwaka huwa mzuri, unaweza kuta mtu umefanya biashara zako sasa unafunga jumla jumla ili ufungue mwaka mwingine.

“Nitajaribu kuongea na Rostam ikiwezekana nitatoka na wimbo wa tunafunga jumla jumla baada ya hii ya Iokote,” alisema Maua Sama. Mitandaoni, Rostam wanaotamba na Wimbo wa Kaolewa, wamebuni staili ya kuweka picha au vipande vya video wakisema tunafunga jumla jumla jambo lililowashika mashabiki wengi na kujikuta kila mtu akitumia usemi huo.

Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.