The House of Favourite Newspapers

Mazingira ya Kifo cha George Michael Yamegubikwa na Utata

george-michael-34 george-michael-1 george-michael-2 george-michael-3 george-michael-4 george-michael-5 george-michael-6 george-michael-7 george-michael-8 george-michael-9 george-michael-10 george-michael-11 george-michael-12 george-michael-13 george-michael-14 george-michael-15 george-michael-16 george-michael-17 george-michael-18 george-michael-19 george-michael-20 george-michael-21 george-michael-22 george-michael-23 george-michael-24 george-michael-25 george-michael-26 george-michael-27 george-michael-29 george-michael-30 george-michael-31 george-michael-32 george-michael-33 george-michael-34 george-michael-35

KIFO cha aliyekuwa mwanamuziki wa Uingereza, Michael George, bado hakijaelezewa kihalisi na wataalam chanzo chake.

Rafiki wa muda mrefu wa mwanamuziki huyo aitwaye Fadi Fawazi (43) alielezea jinsi alivyokwenda nyumbani kwa George na kumkuta amefariki kitandani mwake.

“Tulikuwa twende tukapate chakula cha mchana kwa ajili ya Krismas.  Nilipokwenda kumwamsha, nilikuta tayari kafariki.  Hatujui kilichotokea, kulikuwa kuna matatizo makubwa hivi karibuni, lakini George alikuwa anategemea kusherehekea Krismasi kama mimi,” alisema Fadi.

Aliliambia gazeti la Daily Telegraph: “Sasa kila kitu kimevurugika.  Nataka watu wamkumbuke alivyokuwa, kwani alikuwa mtu mzuri.

Fadi alikuwa pia ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Tweeter kwamba: “Ni Krismasi, sitasahau kumkuta mshikaji wangu amefariki kwa amani kitandani mapema asubuhi.  Daima nitakukumbuka XX.”

Madaktari waliofika kwenye makazi ya mwanamuziki huyo baada ya mwili wake kugunduliwa, walihisi mwanamuziki huyo aliyewahi kuuza zaidi ya rekodi milioni 100 duniani, alifariki kwa ugonjwa wa moyo.

Hata hivyo, polisi wanachunguza kuona iwapo kuna tendo la jinai lilifanyika katika kifo chake, japokuwa hadi sasa hapajaonekana kitu chochote.

Pamoja na yote hayo, Fadi hajahojiwa chochote kama mtuhumiwa katika kifo hicho.  Watu hao wamekuwa wakishirikiana tangu walipoonekana pamoja huko Venice, Italia.
George, ambaye jina lake halisi ni Georgios Kyriacos Panayiotou, aliiteka mioyo ya mashabiki wa muziki kwa muda mrefu, japokuwa katika miaka ya karibuni alikuwa akikabiliwa na tatizo la madawa ya kulevya na kukamatwa kila mara kwa makosa mbalimbali ya uvunjaji wa sheria.

Mwaka jana, binamu wa mwanamuziki huyo aliyekuwa akijihusisha katika mapenzi ya jinsia moja (shoga) alikiri kwamba nduguye huyo aliwahi kulazwa katika kituo kimoja cha kutibu matimizi ya madawa ya kulevya (cocaine) nchini Switzerland.

Katika mazingira hayo, panategemewa kutokea tafrani kuhusu utajiri wa Paundi milioni 100 aliouacha wakati hakuwa na mume, watoto au mtu aliyetegemewa kuwa mrithi.

 

Nay wa Mitego Ametoboa Siri: Hiki ndicho Alichokimiss kwa Shamsa Ford

Comments are closed.