The House of Favourite Newspapers

Mbappe: ‘Jiwe Walilolikataa Cameroon’ Limekuwa Jiwe Kuu la Ufaransa

Kylian Mbappe na baba yake, Wilfried Mbappe.

NYOTA wa Kombe la Dunia ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG ya Ufaransa pia, Kylian Mbappe, aliwahi kukataliwa kuchezea timu ya Cameroon ambapo baba yake alitakiwa kutoa malipo ya fedha ambayo alishindwa kuipata.  Lakini, Ufaransa, nchi ambayo alizaliwa, ilimchukua na kumwingiza katika ulimwengu mkubwa zaidi wa soka,  bure!

Kylian (kulia) na familia yake.

Wilfried Mbappe, baba yake nyota huyo aliwahi kuviambia vyombo vya habari kwamba: “Nilitaka mwanangu achezee timu ya taifa ya Cameroon lakini shirikisho la soka likaniambia nitoe fedha kiasi fulani ambayo sikuwa nayo lakini Ufaransa haikunitaka nitoe wala senti moja.”

 

Mbappe (19) alizaliwa katika kitongoji cha Bondy, jijini Paris, Ufaransa katika familia ya wanamichezo ambapo baba yake alikuwa mcheza soka na kocha, mama yake aitwaye Fayza Lamari, alikuwa mcheza mpira wa mikono (handball).  Vilevile, kaka yake wa kambo, Jires Kembo-Ekoko, ni mcheza soka wa kulipwa ambaye amecheza sehemu mbalimbali duniani, hivyo kumsaidia sana Kylian katika medani ya soka.

 

Mama yake Mbappe, Fayza Lamari, ni mwenye asili ya Algeria, na baba yake ni mwenye asili ya Cameroon, zote nchi za Afrika.

 

Nyota huyo  ambaye aliing’arisha Ufaransa, ni mmoja wa wanasoka mahiri wapatao 15 wenye asili ya Afrika wanaoichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, na hivyo kuifanya iwe na mashabiki lukuki duniani wenye asili ya Afrika.

 

Baba yake Mbappe akiwa jukwaani wakati wa michuano ya Kombe la Dunia.

Mbappe ambaye alikuwa ni mmoja wa wachezaji wadogo zaidi kushiriki michuano hiyo iliyofanyika nchini Urusi, amewashangaza wapenzi wa soka ambao wanasema amekomaa katika soka kabla ya ‘wakati’  wake halisi kutimia.

 

Kylian amejiendeleza kwa kiwango kikubwa kutokana na maarifa ya soka la kulipwa la kaka yake, Jires, hali ambayo imemfanya kucheza soka bila kujali majina ya mastaa wa mchezo huo, akipigania kupata mafanikio zaidi.

 

Mbappé ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili mdogo kiumri kufunga bao kwenye fainali za Kombe la Dunia huku akijinyakulia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia Chipukizi akiwa na jumla ya mabao manne.

Comments are closed.