The House of Favourite Newspapers

Mbaroni kwa Kuua, Kufukia Mwili Shambani

0

POLISI mkoani Pwani inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumwua mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) kwa tuhuma za kumfumania siku ya Machi 10, 2020, maeneo ya Kibindu, Chalinze Mkoa wa Pwani, na kuufukia mwili huo katika shamba la mahindi.

Watu hao ni  Chacha Machangu aliyeshirikiana na  ndugu zake Emmanuel Chacha Machangu na Hamis Chacha Machangu.

Taarifa ya polisi inasema Chacha Machangu (27) alimfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine na alimshambulia kwa kumkatakata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majeraha yaliyosababisha chake Machi 10, 2020.

Baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kwa ridhaa yao walionyesha mahali shimo lilipo ambapo mwili ulipatikana na kufanyiwa uchunguzi na daktari na baadaye kuzikwa.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani.

 

WAHAMIAJI WAKAMATWA

POLISI mkoani Pwani, kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 51, raia wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini kupitia bandari bubu ya Makurunge katika wilaya ya Bagamoyo.

Idadi hiyo inafikia wahamiaji haramu 100 baada ya wengine 49 kukamatwa juzi, Kidomole, Fukayose. Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa, alisema raia hao wamekabidhiwa kwa vyombo vya dola kwa taratibu za kisheria.

 

AKAMATWA AKISAFIRISHA BANGI

Pia, polisi Wilaya ya Kibaha, Pwani,  inamshikilia Ally Hashimu Athumani mkazi wa Malela, Morogoro,  kwa kosa la kusafirisha viroba vitano vya bangi.

Taarifa ya polisi Wilaya ya Kibaha, Pwani, inasema Machi 20, 2020 majira ya saa 12:00 huko maeneo ya Maili Moja, walimkamata mtuhumiwa huyo akisafirisha kiasi hicho cha bangi kutoka Morogoro kuelekea Dar es Salaam kwa kutumia gari yenye namba za usajili T.688 CZK Toyota Carina nyeupe.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

 

 

Leave A Reply