The House of Favourite Newspapers

MBASHA AFUNGUKA KUHUSU KUTELEKEZA WATOTO WAKE

0

MWIMBAJI wa Injili Tanzania

MWIMBAJI wa Injili Tanzania, Emmanuel Mbasha, ameamua kuvunja ukimya juu ya tuhuma alizopewa za kutelekeza watoto aliozaa na wanawake tofauti na kusema habari hazina ukweli wowote ule.

Akihojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mbasha amesema tuhuma hizo ni uongo na anachukia watu wanaotengezea habari hizo, kwani yeye hahitaji habari za kutunga ili kupata kiki kwa kuwa yeye si mwanamuziki wa Bongo Fleva.

“Si kweli, hivyo vitu ni vya uongo tena nakanusha kabisa. Hivi kwa nini vitu vingi vinaongelewa vya uongo? Sipendi uongo, hivyo ni vitu vya Bongo Fleva bhana, mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelea vitu ambavyo havina faida,” alisema Emmanuel Mbasha.

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba Emmanuel Mbasha amewazalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza, kisha kukimbilia kwa mwanamke mmoja mwenye uwezo kipesa hapa mjini Dar es Salaam na kuweka kambi hapo na huyo mwanamke mpya.

NA SAMSON JEREMIAH

Leave A Reply