Mboni Kuanika Ndoa Yake

BAADA ya kukaa kimya kwa muda huku yakisemwa mengi kuhusu ndoa yake, mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba ameibuka na kusema ataanika kila kitu hivi karibuni.

 

Mboni Masimba inasemekana alifunga ndoa Septemba 6, 2019 na Mwanaume anayefahamika kwa jina la Ally Tajiri, ambaye imeelezwa kuwa ni mpenzi wake wa muda mrefu. Ndoa hiyo ilifungwa Masaki jijini Dar es Salaam.

 

Akipiga stori na Amani, Mboni alisema anajua kwamba mengi yamezungumzwa kumhusu yeye lakini atakapofunguka kila mtu atapata mbivu na mbichi kuliko watu kuendelea kuamini yaliyozungumzwa.

 

“Wakae tu mkao wa kula, nitaeleza kila kitu,” alisema Mboni.

Ndoa ya Mboni ilifanyika kwa usiri ambapo yaliibuka maneno mengi huku wengine wakidai kuwa ameolewa na aliyekuwa bwana wa rafiki yake.

Stori: Hamida Hassan, AMANI


Loading...

Toa comment