The House of Favourite Newspapers

Mbunge Bobi Wine Kufikishwa Mahakama ya Kijeshi Leo

MBUNGE Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina Bobi Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu Kaskazini mwa Uganda. Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.
Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.

 

Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin, Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa.
Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wamekanusha. Mbunge huyo anatarijiwa kufikishwa mahakamani kwa madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria pamoja na tuhuma za wafuasi wake kuushambulia msafara wa Rais Museveni.

Comments are closed.