The House of Favourite Newspapers

Halima Mdee Ashikiliwa na Polisi Oyster Bay

Halima Mdee.

MBUNGE  wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, anashikiliwa na polisi katika kituo cha Oyster Bay, kufuatia agizo la Mahakama ya Kisutu la kukamatwa kwa wabunge wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 

 

Jeshi la Polisi Kinondoni limesema Mdee ameripoti mwenyewe kituoni hapo leo Novemba 16, 2019 na atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

“Ni kweli yupo hapa kituoni tunamshikilia kama ambavyo Mahakama iliagiza na yeye amekuja mwenyewe kuripoti hapa, hivyo taratibu zote za kipolisi zinafanyika na Jumatatu atafikishwa mahakamani,” amesema Msaidizi wa RPC Kinondoni.

 

Amri hiyo ya kukamatwa kwa wabunge hao Halima Mdee, Peter Msigwa, John Heche na Ester Bulaya, ilitolewa jana, Novemba 15, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, ambapo alisema kuwa kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa mashtaka kumhoji Mbowe na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake kutoka upande wa utetezi na ndipo ilipobainika washtakiwa hao wanne kutowepo mahakamani.

Comments are closed.