Mchezaji wa Man City Gvardiol Aingia Kambini na Maafisa wa Vikosi Maalum

Wakati wachezaji wengi duniani wakirudi kwa mazoezi mepesi ya uwanjani, beki wa Manchester City, Joško Gvardiol, ameanza msimu mpya kwa njia ya kipekee kabisa. Akiwa nyumbani Croatia, Gvardiol alishiriki mazoezi ya Kikosi maalum Jeshini, yaliyotengenezwa kwa raia.
Mafunzo hayo yaliyofanyika porini yalisimamiwa na wanajeshi wastaafu wa vikosi maalum na wataalamu wa usalama binafsi. Yalijumuisha majaribio makali ya uvumilivu, changamoto za uhai wa kikundi na mikakati ya kusonga kijeshi. Mpango huu umetengenezwa mahususi kama njia ya kuinua uwezo wa kimwili na kiakili kwa watu wanaotaka kujisukuma hadi mwisho wa uwezo wao.


Comments are closed.