The House of Favourite Newspapers

MCHUNGAJI ALIYEMTOA GEREZANI AMBER RUTTY TUMUELEWEJE?

Mchungaji Mashimo na Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’

WAKATI zile video zinazomuonesha mwanamuziki Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ akifanyiwa vitendo vya ulawiti zilipovuja, wengi walionesha masikitiko yao. Baadhi walikuwa wakijiuliza kwamba ilikuwaje mpaka mrembo huyo akakubali kufanyiwa kitendo hicho na kurekodiwa?  

 

Hakika hakuna aliyepata majibu sahihi. Wapo waliosema eti ilikuwa ni kiki, lakini sababu hiyo wala haiingii akilini kabisa. Utafute kiki kwa kujionesha ukifanyiwa ufirauni kama ule, kiki hiyo itakusaidia nini ikiwa tayari umeshadharaulika huku pia ukiwa umeathirika kiafya?

 

Hiyo ikawa haijawaingia akilini walio wengi. Wengine wakasema, ni pombe. Kwamba wakati wanafanya ule mchezo akili zilikuwa zimewaruka kwa sababu walilewa. Sababu hiyo kidogo ‘inakliki’ kwa sababu mtu na akili zake timamu hawezi kufanya vile halafu akajirekodi.

 

Hakika yamesemwa mengi lakini mwisho wa siku sheria ikachukua mkondo wake na wengi wakasema ni bora waadabishwe ili iwe fundisho kwa wengine. Amber Rutty na bwana wake aitwaye Said Mtopali wakatiwa mbaroni, wakapandishwa kizimbani na wakatupwa gerezani baada ya kukosa dhamana.

 

Wamekaa gerezani kwa takribani siku 25, kama ni cha mtemakuni watakuwa wamekiona licha ya kwamba kesi bado inaendelea. Hata hivyo, katika kuonesha kwamba, wengi hawakufurahishwa na kile walichokifanya, katika siku za mwanzo ambazo walikuwa wakifikishwa mahakamani, hakuna aliyejitokeza kuwachukulia dhamana.

 

Hiyo huenda ilichangiwa na mambo haya; kwanza labda hawakuwa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa na uwezo wa kutimiza masharti ya dhamana. Pili; yawezekana kwa walichokifanya watu wengi walikasirika, wakaona wawaache ili wakomeshwe.

 

Nikiri tu kwamba, sikufurahishwa na kile walichokifanya lakini nilikuwa nawaonea huruma sana kwa sababu nilihisi hata wao wenyewe baada ya video kuvuja ndiyo wakazinduka kwamba kumbe walifanya jambo baya. Walionekana ni wenye kujutia walichokifanya.

 

Huruma yangu iliongezeka kwao baada ya kusikia historia ya Amber Rutty iliyotolewa na baba yake, Mzee Abubakary Abdul Milenga, kisha mzee huyo anayeishi Bomba Mbili, Songea kueleza kuwa, alitamani sana kufika Dar kumuwekea dhamana mwanaye lakini alishindwa kwa kuwa hana uwezo. Hapo ndipo nilipotamani kujitoa kwenda mahakamani kumuwekea dhamana bila kujali watu wangesema nini juu yangu.

 

Bahati mbaya sana na mimi nikakosa vigezo lakini nikafarijika kusikia kuwa, Mchungaji wa Kanisa la Emmaus Bible Church lililopo Mbezi Louis jijini Dar amejitoa kwenda kumuwekea dhamana msanii huyo. Wengi hawakuamini taarifa hiyo na wapo waliofikia hatua ya kusema kuwa, mtumishi huyo wa Mungu anatafuta kiki tu na asingeweza kufanya hivyo.

Tofauti na matarajio ya wengi, juzi Jumanne mtumishi huyo alitimiza kile alichokisema, akamtolea dhamana mtuhumiwa huyo na sasa yuko uraiani huku kesi yao ikiendelea. Baada ya mchungaji huyo kufanya jambo hilo, wapo waliomsema vibaya kwamba, ina maana yeye kafurahishwa na kile kilichofanywa na msanii huyo hadi kuamua kwenda kumuwekea dhamana?

 

Mimi kupitia makala ambacho tunatakiwa kujifunza kupitia kile alichokifanya. Ukweli ni kwamba, kila mtu ana udhaifu wake, kila mtu ana dhambi. Hakuna ambaye ametakasika kwa asilimia zote. Ni kweli Amber Rutty amekosea ila haikuwa sawa wale ambao walikuwa na uwezo wa kumuwekea dhamana kumkaushia eti kwa kuwa alichokifanya kinachefua. Ilitakiwa kutumika ubinadamu tu, kwamba asaidiwe kisha huenda akitoka atajifunza.

 

Alichokifanya mtumishi Mashimo kitupe fundisho kwamba, wanaofanya makosa wana nafasi kubwa ya kusaidiwa katika kubadilika. Kama alivyosema Mashimo kwamba yeye anahubiria hata makahaba, basi tusije kushangaa hata Amber Rutty ambaye inadaiwa aliokoka akiwa gerezani, kesi yake ikiisha akawa mtu mwema.  Ipo mifano ya watu wengi sana ambao walifanya mambo machafu huko nyuma lakini leo hii ni watu safi, wameokoka, wanahubiri neno, wanakuwa chachu ya wengine kubadilika.

 

Hivyo basi, watu kama akina Amber Rutty wanapotokea kwenye jamii  yetu, tusiwanyanyapae, tusiwatenge bali tuwe nao karibu na kuhakikisha tunawatoa kwenye mambo hayo ambayo hayafai katika nchi iliyostaarabika kama ya Tanzania. Pia nichukue fursa hii kumshukuru Mchungaji Mashimo kwa alichokifanya. Ameonesha utumishi wake kwa Mungu lakini pia ametumia fursa hiyo kuitangaza huduma yake na kanisa lake.

 

Sasa hivi watu wengi wanasubiri kuona kama kweli binti huyo kaokoka au ni maneno tu. Watu wanaona ugumu katika hilo kwa sababu baba wa binti huyo ni shehe na amejinasibu kuwa kamlea binti yake huyo kwenye misingi ya dini. Je, msaada aliopewa na mchungaji Mashimo unaweza kuwa sababu ya yeye kuingia kwenye ukristo? Acha tusubiri tuone pale ambapo Amber Rutty atatinga kanisani na kuamua kumpokea Bwana Yesu.

Na Amran Kaima.

ITAKULIZA! Mke wa AZORY Apata PIGO Lingine, Asimulia kwa Uchungu!

Comments are closed.