The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Anaswa na Denti Kichakani

 

DAR ES SALAAM: Hii ni aibu iliyoje? Hebu vuta picha mtu mwenye heshima yake kwenye jamii kama mchungaji, halafu anaingia tamaa kwa kabinti kadogo na kukashawishi kisha kwenda nako kichakani kufanya naye mapenzi.

Hakika hii ni zaidi ya aibu ambayo inadaiwa kumkumba mchungaji wa kanisa moja maeneo ya Msigani, Kata ya Wazo-Hill jijini Dar anayetajwa kwa jina la Mchungaji Sixbert.

Awali, baada ya kunaswa ‘live’ kichakani na kabinti hako ambaye ni denti wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14, wananchi wenye hasira kali walitaka kumtembezea kichapo, lakini bahati nzuri, wasamaria wema walishauri kumfikisha kwa mwenyekiti wa mtaa na baadaye akabebwa msobemsobe hadi Kituo cha Polisi cha Wazo-Hill kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kililiambia Gazeti la Ijumaa kuwa, mchungaji huyo, awali alikuwa na uhusiano wa karibu na familia ya mwanafunzi huyo ambapo walifikia hatua ya wazazi hao kumruhusu kwenda kulala nyumbani kwake kwani naye ana familia yake.

“Ilisemekana mchungaji huyo alitumia mwanya huohuo kufanya yake.

“Akiwa anaishi naye, alianza taratibu kumfundisha mchezo mbaya binti huyo, ambapo kuna wakati wazazi walianza kushtukia mchezo na walipomuuliza binti huyo alikataa katakata,” kilieleza chanzo hicho.

SIKU YA TUKIO…

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, baada ya wazazi kumhisi mchungaji huyo, walilazimika kuwa makini ambapo siku ya tukio, denti huyo, akiwa nyumbani alitoweka ghafla na baada ya mchungaji huyo kuonekana akielekea kwenye kichaka kilicho na jirani na eneo la makazi.

“Tulipoona mchungaji amekatiza kuelekea kichakani na mtoto naye akatoweka, tukajua tu ndiyo muda wa yeye kufanya uchafu wake, tukamfuatilia mpaka kwenye kichaka na hamadi tulipofika kwenye korongo lililopo jirani na maeneo hayo, tukamnasa mchungaji laivu akivunja amri ya sita na kabinti ambako ni denti wa shule ya msingi,” kilisema chanzo.

BABA AFUNGUKA

Kufuatia sakata hilo kuwa kubwa, wanahabari wetu walikwenda nyumbani kwa wazazi wa mwanafunzi huyo na kumkuta baba yake, Mussa Said ambaye baada ya kumuuliza kulikoni juu ya sakata hilo alianza kufunguka;

“Mimi huyu mchungaji ambaye huwa anatoa huduma za kichungaji nilikuwa nikimuamini sana kufikia kumuachia binti yangu akalale kwake. Sikuwa na shaka naye kwa kuwa anaishi na mkewe, sikujua kama hayo yangetokea.

SAA MBILI KASORO USIKU…

“Tukio lenyewe lilitokea Septemba 24, mwaka huu majira ya saa mbili kasoro usiku ambapo tukiwa hapa nyumbani na familia yangu alipita mchungaji akiwa katika hali ya kimachale. Japokuwa kulikuwa na giza, lakini niliweza kumuona vizuri.

“Baada ya kupita dakika kidogo, binti yangu naye akatoweka, ndipo tukaanza kumsaka mpaka tulipomnasa mchungaji kwenye kichaka korongoni akifanya ufuska na binti yangu ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita. Kama mzazi, roho iliniuma sana aisee,” alisema mzazi huyo kwa uchungu.

WAMPELEKA KWA MWENYEKITI

Akizidi kusimulia tukio hilo huku akiwa kwenye masikitiko mazito, alisema baada ya kumkuta eneo la tukio kwa kushirikiana na majirani, walifanikiwa kumkamata na kumpeleka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Nyakasangwe, Peter Bilebela.

“Tulishirikiana na majirani kumkamata na kumpeleka kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ambaye aliwapigia simu polisi ambapo tulikwenda kutoa maelezo na kumfungulia kesi ya kufanya mapenzi mwanafunzi katika jalada namba MDL/ RB/4929/2019, namuomba Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa atusaidie ili sheria ichukue mkondo wake,” alimalizia mzazi huyo.

MAMA MZAZI ANENA

Baada ya kuzungumza na baba huyo, wanahabari wetu walizungumza na mama wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Mhanzi ambaye alisema uhusiano kati ya mwanaye na mchungaji huyo ulianza muda mrefu ambapo alishamuonya mno binti yake baada ya watu kumtonya, lakini binti huyo alikuwa akikataa.

“Siku moja binti yangu alichelewa kurudi nyumbani na kufika usiku sana, baba yake alipoanza kumchapa, mchungaji huyo alitokea kusikojulikana na kuanza kumzuia binti huyo asipigwe.

AMKINGA KWA MGONGO WAKE…

“Baba wa mtoto huyo alipozidi kumchapa binti yetu, mchungaji huyo aliweka mgongo achapwe yeye upendo ambao nao ulizidi kututia shaka,” alisema mama wa mtoto huyo.

JIRANI NAYE ANENA

Naye jirani aliyeshuhudia tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Josephat Johnson, alisema siku ya tukio alipigiwa simu na baba wa mtoto huyo aliyemwambia kuwa binti yake ambaye amekuwa akimtilia shaka muda mrefu kutembea na kiongozi huyo wa dini, alikuwa ametoweka nyumbani muda mfupi baada ya mchungaji huyo kupita, hivyo alihisi alikuwa amemfuata wakafanye yao.

“Baada ya kuniambia, tuliwafuatilia kwa kuwatafuta sana mpaka tulipowabamba huko mabondeni kwenye kichaka, mchungaji akiwa ameshusha suruali huku wakifanya yao,” alisema jirani huyo.

HUYU HAPA MWENYEKITI

Katika kuzidi kufuatilia habari hiyo, wanahabari wetu walizungumza na mwenyekiti Bilebela ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kusema alifanya jitihada kubwa za kumuokoa mtuhumiwa huyo kwenye mikono ya wananchi wenye hasira waliokerwa na kitendo hicho.

“Nawapa onyo wazazi wenye tabia ya kuwaruhusu watoto zao kwenda kulala kwa watu wengine maana nasikia huyo awali alikuwa akilala kwa huyo kiongozi wa dini kabla ya wazazi kushtuka na kumchukua binti yao,” alisema mwenyekiti.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mtumishi huyo wa Mungu alikuwa mikononi mwa polisi akisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi.

Gazeti la Ijumaa linaahidi kufuatilia sakata hili ili kujua nini hatma yake? Usikose mwendelezo wake!

Stori: Stori: Richard Bukos na Neema Adrian, Ijumaa

Comments are closed.