The House of Favourite Newspapers

MEGHAN MARKLE NA HARRY WANATARAJIA MTOTO

Prince Harry, Duke of Sussex and the Duchess of Sussex in the Ascot Landau carriage during the procession after getting married
Meghan na  Harry

Meghan Markle, mkewe Mwanamfalme wa Harry nchini Uingereza ni mjamzito na anatarajiwa kujifungua mwaka ujao wa machipuko, kasri la Kensington limefichuwa. Tangazo hilo linajiri wakati Meghan, mwenye umri wa miaka 37, na mwanamfalme Harry, mwenye miaka 34, waliofunga ndoa huko Windsor miezi mitano iliyopita, waliwasili Sydney Jumatatu katika kuanza kwa ziara ya siku 16 nchini Australia na New Zealand.

Kasri la Kensington limesema wanandoa hao wana “furaha kutangaza habari hii njema kwa umma”.Mtoto wao atakuwa wa saba katika orodha ya ufalme. Malkia na maafisa wengine wa ufalme waliambiwa kuhusu habari hizo njema siku ya Ijumaa, wakati familia ya kifalme ilipokusanyika Windsor kwa harusi ya mwanamfalme Eugenie. Fununu hizo zilizidi alipoonekana kujiziba kwa bahasha mbili kubwa tumboni alipowasili Sydney, katika ziara yao rasmi ya kwanza tangu walipooana, ambayo ilifanyika katika kanisa la St George’s huko Windsor.

Credit : Bbc swahili

Comments are closed.