The House of Favourite Newspapers

‘Meneja wa Dangote Auawa kwa Kutoa Fedha Ndogo Kufidia Mateka’

bello-man-696x696

Istifanus Bello enzi za uhai wake.

WATU watatu wanaodaiwa kumteka na kumwua meneja raslimali watu wa kampuni ya Dangote Industries Limited, Istifanus Bello, wamesema aliawa kwa kutoa fedha ambayo haikutimia kama fidia kwa ajili ya kuachiliwa watu waliokuwa wametekwa.

Watuhumiwa hao,  Abdullahi Saliu, Babuga Adamu na Abubakar Gide, waliliambia gazeti la PUNCH Metro kwamba Bello aliwaudhi baada ya kuwapelekea Naira milioni 5.6 badala ya Naira milioni 10m zilizokuwa zimekubaliwa kwa ajili ya kuachiliwa kwa wataalam wanne wa kigeni wa kampuni hiyo waliokuwa wametekwa na kundi la watu hao.

dangote-staff-killers-kidnappersWatuhumiwa.

Walisema Bello aliuawa baada ya kushikiliwa kwa siku tatu kwani anadaiwa alikataa kumpigia simu mwajiri wake ili alipe kiasi kilichokuwa kimebakia cha Naira milioni 4.

Kabla ya hapo, PUNCH Metro lilikuwa limeripoti kwamba Bello alikuwa amekwenda eneo la  Ijebu-Igbo, Jimbo la Ogun, akiwa na Naira milioni  5.6 kama fidia ili kuwakomboa mateka hao.

Wakati wataalam hao wa kigeni waliachiliwa, yeye alikamatwa na kuuawa baadaye ambapo mwili wake uliripotiwa kupatwa na polisi katika mto mmoja.

ooUchunguzi ulioendeshwa na Timu ya Kiitelijensia chini ya Inspekta Jenerali wa Polisi Abba Kyari, ulisababisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao – Saliu, Adamu na Gide — jijini Lagos, na katika majimbo ya Kwara na Ogun.

Watuhumiwa hao waliokuwa wafugaji wa kabila la Wafulani, Jumanne wiki hii walihamishwa kutoka makao makuu ya kikosi hicho jijini Abuja na kupelekwa katika kikosi maalum cha kupambana na wizi huko Ikeja, lagos, ili kusubiri upelelezi ukamilike.

Business magnate man Aliko Dangote, ranked by Forbes Magazine as the richest man in Africa, speaks during a send off ceremony of 250 Nigerian health workers on a mission to fight Ebola virus in affected West African countries and launch of African initiative operating under the hash tag #AfricaAgainstEbola in Lagos on December 3, 2014. Two hundred and fifty volunteer Nigerian medical corps under the auspices of the African Union Support to Ebola Outbreak in West Africa (ASEOWA) were given a send off to fight Ebola Virus Diseases in the affected three West African countries of Liberia, Sierra Leone and Guinea. The African Union, which is collaborating with the private sector to raise funds to support and strengthen the Unions response to the crises, is sending more than 1000 health workers before Christmas. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI (Photo credit should read PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images)Aliko Dangote

Katika mahojiano maalum na mwandishi wetu, watuhumiwa hao waliokuwa anazungumza katika lugha ya Kiyoruba, walisema watu 10 wa kundi lao ndiyo walioendesha oparesheni hiyo.

Saliu, mwenye umri wa miaka 20, mweneji wa Jimbo la Kano, alisema kundi hilo lilikuwa linaongozwa na Alti ambaye alifyatua risasi iliyomuua Bello.

PUNCH Metro liligundua pia kwamba watuhumiwa hao waliutupa mwili wa Bello katika mto na kuufungia gogo kubwa kuzuia usielee.

Kwa mujibu wa polisi, upelelezi kuhusu tukio hilo, bado unaendelea.

MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.