The House of Favourite Newspapers

Mfahamu Mwanamke Asiyehisi Maumivu Mwilini!

 

JO CAMERON  aligundua kuwa ngozi yake inaungua pale alipohisi  harufu ya kuungua kwa ngozi yake. Mara nyingi mikono yake huungua kwenye jiko la kuokea chakula, lakini huwa  hahisi maumivu ya kumpa tahadhari kuwa yuko hatarini.

 

Mwanamke huyo ni mtu wa pili duniani kuwa na hali hii ya mabadiliko ya kijenetiki ambayo hutokea kwa nadra sana. Inamaanisha kuwa Cameron huwa hahisi maumivu kabisa, hana wasiwasi wala huwa hapati hofu.

 

Hali ilikuwa hivyo mpaka alipotimiza miaka 65, ndipo alipogundua kuwa yuko tofauti  — pale madaktari waliposhindwa kuamini kuwa hahitaji dawa za kuondoa maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

 

Alipofanyiwa upasuaji kwenye mkono wake, madaktari walimtahadharisha kuwa ategemee kupata maumivu baada ya upasuaji lakini  hakuhisi maumivu ydyote.   Daktari wake wa dawa za usingizi, Devjit Srivastava, alimpeleka kwa wataalamu wa masuala ya maumbile na jenetiki katika chuo cha London na Oxford.

 

Baada ya vipimo, walibaini kuwa ana mabadiliko kwenye vinasaba vyake vinavyomfanya asihisi maumivu kama ilivyo kwa watu wengine.

 

Mama huyo  aliliambia shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa madaktari hawakumwamini alipowaambia hahitaji dawa ya kuondoa maumivu baada ya upasuaji.

 

Alisema: ”Tulizungumza kabla ya kwenda kwenye chumba cha upasuaji na nikawahakikishia kuwa sitahitaji dawa za kuondoa maumivu.

 

”Datari alipogundua kuwa sikuwahi kumeza dawa za maumivu, alitazama historia yangu ya kitabibu na kugundua kuwa sikuwahi kutumia dawa za kuondoa maumivu.”

 

Hilo lilimanya apelekwe  kwa wataalamu nchini Uingereza. Ilipobainika,  alijua kwamba kumbe hakuwa na ”afya njema”  kama ailivyokuwa akiamini.

 

Alisema:”Nikikumbuka huko nyuma, nikagundua sikuwahi kuhitaji dawa za kuondoa maumivu, lakini kama huzihitaji huwezi kuhoji kwa nini huhitaji.

 

”Wewe ni wewe ulivyo mpaka pale mtu mwingine atakapobaini vinginevyo. Nilikuwa mwenye furaha ambaye sikubaini kama kuna tofauti yoyote mwilini mwangu.”

 

Hakuwahi kupata maumivu hata wakati anajifungua, ambapo anasema:  ”Halikuwa jambo la kawaida, lakini sikuwa na maumivu. kwa kweli niliifurahia hali hii.”

 

Madaktari waliamini kuwa atakuea na uwezo wa kupona haraka  kuliko kawaida kwani jeni zake pia zinamfanya asahau na asiwe mwenye hofu

 

”Zinaitwa jeni zenye kuleta furaha au zinazosahau.   Nimekuwa nikiwaudhi wengine kwa kuwa na furaha na mwenye kusahau maisha yangu yote,” alieleza.

 

Alisema hivi karibuni alikuwa na uvimbe mdogo baada ya kujigonga akiwa kwenye gari, lakini hali hiyo ambayo wengi wangeiona mbaya sana, haimkumshtua hata kidogo.

 

”Sina adrenalini. Lazima uwe nayo ili iweze kukupa tahadhari kuhusu hali ulionayo, ni sehemu ya hali ya binadamu, lakini siwezi kubadili hali hii,” anasema.

 

 

Watafiti wanasema inawezekana kuna watu wengine kama  yeye ambapo mmoja kati ya wagonjwa wawili baada ya upasuaji hupata maumivu kidogo au maumivu makali, pamoja na kuwepo kwa uboreshwaji wa dawa za kuondoa maumivu.

 

Aliyoyapitia Cameron yamo kwenye maandiko ya utafiti wa British Journal of Anaesthesia, yaliyoandikwa na madaktari Srivastava na Dokta James Cox

 

 

Comments are closed.