The House of Favourite Newspapers

Mfanyabiashara Maarufu wa Rwanda Auawa Msumbiji

KIONGOZI wa umoja wa Wanyarwanda waishio nchini Msumbiji (diaspora), Louis Baziga,  mepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo.

 

Maofisa wanasema Baziga alikuwa ndani ya gari lake juzi (Jumatatu) mchana ambapo baada ya kuondoka nyumbani kwake Matola,  alikumbana na watu waliokuwa na bunduki.

 

Baziga alifahamika kuwa mfuasi wa serikali ya Rwanda na alikuwa mfanyabiashara mkuu aliyeendesha biashara ya maduka na duka la kuuza dawa huko Maputo.

 

Claude Nikobisanzwe, Balozi wa Rwanda nchini Msumbiji, amesema  waliompiga risasi Baziga, walitoweka kabla ya kutambulika.

 

“Bwana Baziga alikimbizwa hospitalini lakini ikaarifiwa kwamba ameshafariki alipowasili. Polisi wameanza uchunguzi; ni mapema mno kujua kwa nini ameuawa,” Nikobisanzwe amesema.

 

Tangu 1994, mataifa ya kusini mwa Afrika yamewahifadhi maelfu wa raia wa Rwanda – wakimbizi na wahamiaji wa halali.

 

Inaaminika kwamba zaidi ya watu 5,000 kutoka Rwanda wanaishi Msumbiji.

 

Kumekuwa na mauaji katika eneo hilo dhidi ya wakosoaji wa chama tawala nchini Rwanda wanaoishi uhamishoni, na hivyo  inatuhumiwa kwamba watu hao ndiyo wanaolengwa na utawala uliopo.

 

Mnamo Oktoba 2012, Théogène Turatsinze, mfanyabiashara nchini Msumbiji na aliyekuwa kiongozi wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Rwanda alitekwa.

 

Na mnamo Mei, Camir Nkurunziza, aliyekuwa mlinzi wa kitengo cha ulinzi wa rais, alipigwa risasi mjini Cape Town, Afrika Kusini, ambapo polisi walisema alihusika katika wizi wa gari.

 

Louis Baziga ni nani?

Baziga alihamia nchini Msumbiji miongo kadhaa iliyopita kufuatia mauaji ya kimbari yaliotokea Rwanda mwaka 1994.

 

Alikuwa kiongozi wa jamii ya Wanyarwanda wanaoishi uhamishoni na alikuwa na uhusiano wa karibu na ubalozi wa nchi hiyo.

 

 

Comments are closed.