The House of Favourite Newspapers

MGOMO WA MADREVA WATIKISA MBEYA

 

Madereva wa daladala jijini Mbeya wamegoma kusafirisha abiria kuanzia alfajiri ya leo Jumatatu, Machi 18, 2019 kwa kile walichokilalamikia madereva wenzao wa bajaji kufanya usafirishaji kwenye barabara kuu na kupelekea wao kukosa mapato.

Usafiri unatumika kwa sasa ni bodaboda, gari ndogo za kubeba mizigo maarufu ‘kirikuu’, bajaji pamoja na Noah.

Baada mgomo huo Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani limefika kwenye vituo kutoa msaada kwa wanafunzi kwa kusimamisha mabasi yanayotoka Kyela na Iringa ili kuwasafirisha wanafunzi.

Comments are closed.