Mgunduzi wa e-mail, Ray Tomlinson afariki dunia

mail (1)
Ray Tomlinson enzi za uhai wake.

RAY Tomlinson, raia wa Marekani, ambaye ndiye aliyevumbua utumaji wa barua pepe kwa Kiingereza e-mail amefariki dunia.

mail (2)

Tomlinson amefariki akiwa na umri wa miaka 74.
Mgunduzi huyu aliibuka na wazo la kutuma ujumbe wa kieletroniki kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia mitandao mbali mbali mwaka 1971.

Aliandika ujumbe wa kwanza wa barua pepe wakati akifanya kazi Boston, kama Mhandisi wa kompyuta.

ray-tomlinson-color

Pia alikuwa mwanzilishi wa matumizi ya alama “at”(@)kuwa ndio alama kuu ya utumaji wa barua pepe.
Wakati wa uhai wake Tomlinson alisema hawezi kukumbuka barua pepe yake ya kwanza ilielezea nini.

Toa comment