The House of Favourite Newspapers

Mibao ya Molinga Yanga Yaibua Mijadala

DAVID Molinga, mshambuliaji wa Yanga, mibao yake anayofunga kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara inafi kirisha kutokana na aina yake na matokeo ambayo timu yake inayapata.

 

Molinga amefunga mabao matatu katika Ligi Kuu Bara ambayo yana rekodi yake huku mawili akiyafunga kwa mtindo mmoja na yote amefunga Uwanja wa Uhuru.

 

Takwimu zinaonyesha kwamba akishafunga yeye hakuna mchezaji mwingine wa Yanga anayefunga hadi mchezo unamalizika. Bao lake la kwanza alifunga Uhuru wakati Yanga ikilazimisha sare ya mabao 3-3 na Polisi Tanzania ambapo alifunga akiwa ndani ya 18 kwa kichwa akimalizia pasi ya Mrisho Ngassa na bao lake la pili alifunga kwa mpira wa adhabu uliozama moja kwa moja ndani ya lango.

 

Bao lake la tatu alifunga juzi Uhuru mbele ya JKT Tanzania na Yanga ilishinda mabao 3-2 na kusepa na pointi tatu jumla na bao lake alifunga kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18.

 

Kwenye mabao yake yote matatu, Molinga amekuwa ni mkomelea nyundo wa mwisho kwa timu yake ya Yanga kwani akifunga kazi inaishia hapo. Yanga imecheza jumla ya mechi sita, imejikusanyia jumla ya pointi 13, huku ikifunga mabao tisa, imefungwa mabao sita ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo kabla ya mechi za jana.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka

BINTI MLEMAVU ANAYEANDIKIA ULIMI AKIRI – “NINA MPENZI, ANATAKA KUNIOA, Kuhusu MIMBA Mh”

Comments are closed.