The House of Favourite Newspapers

Michael Jackson Aongoza Vipato Mastaa Waliofariki

Image result for michael jackson

STAA wa muziki duniani, Mmarekani hayati Michael Jackson, ametajwa kuongoza kwa mwaka wa sita mfululizo orodha ya mastaa waliofariki lakini wakingali wanaingiza mkwanja kutokana na kazi zao walizoziacha.  

Mfalme huyo wa Pop, mwaka jana aliingiza  Paundi milioni 313 (Sh. mil. 930) ikiwa ni sehemu ya mauzo ya muziki wake na kampuni ya EMI, kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Michael aliyefariki mwaka 2009 kutokana na kuzidisha kipimo cha dawa za tiba, hivi sasa ameingiza Paundi bil. 1.8 tangu afariki.

Anayefuatia katika orodha hiyo ni Elvis Presley ambaye aliingiza Paundi mil. 31 kati ya Oktoba 1, 2017 na Oktoba 1, 2018.

Anayeshika nafasi ya tatu ni mcheza ‘golf’, Arnold Palmer aliyeingiza Paundi mil. 27, Charlie Brown, msanii wa katuni akiwa wa nne kwa Paundi mil. 26 na Bob Marley wa tano kwa Paundi mil. 18.

Image result for michael jackson

Mtunzi wa vitabu,  Dr Seuss, ni wa sita (Paundi mil. 12) akifuatiwa na mwasisi wa jarida la Playboy,   Hugh Hefner (Paundi mil. 11.7).  Aliyekuwa mcheza sinema wa kike, Marilyn Monroe, ni wa nane (Paundi mil. 11)

Walifuatia wanamuziki Prince na John Lennon (Paundi mil. 10 na Paundi 9) kila mmoja kwa mfuatano ambapo rapa XXXTentacion aliyeuawa huko Florida mwaka huu mwezi Juni akiwa na umri wa miaka 20 anashika nafasi ya 11 kwa Paundi mil. 8.5.

Waliokamilisha orodha hiyo ya matawi ya juu ni bondia Muhammad Ali (Paundi mil. 6 ) na mwanamitindo Bettie Page (Paundi mil. 5).

Comments are closed.