The House of Favourite Newspapers

Michelle, Sasha Obama Wapamba Shoo ya Beyonce, Jay-Z

 

UHUSIANO wa wanamuziki nguli wa Marekani, Beyonce na Jay-Z,   na familia ya Obama unazidi kuimarika baada ya  Michelle na Sasha kujitokeza katika shoo ya nguli hao ijulikanano kama “On the Run II” inayobamba hivi sasa huko Ufaransa  na iliyofanyika jana (Jumapili) katika dimba la Stade de France ambako waliungana na mama wa Beyonce aitwaye Tina Knowles, wakati Jay alipokuwa akitumbuiza jukwaani.

Mwaka 2014 Michelle aliwapa tafu wanamuziki hao huko Chicago wakati wakiwa katika shoo ya ‘masafa marefu’ kama hiyo ya sasa.

 

Comments are closed.