The House of Favourite Newspapers

Mila na Desturi Zetu Zinampa Nguvu Sana Mwanamke Kuliko Mwanaume

0
Mwanaharakati na Mume wa Joyce Kiria, Aron

KITENDO cha wanaume kunyanyaswa na wake zao halafu wanashindwa kusema kinatokana na ile hali au kasumba ya kuamini mwanaume katika familia hawezi akaonewa lakini pia mila na desturi zetu kama watanzania zinampa nguvu zaidi mwanamke kuliko mwanaume pale inapotokea mwanamke ananyanyasika basi sauti inapazwa sana kuliko pale ambapo mwanaume ananyanyaswa na mwanamke.

 

Katika jamii ya sasa unyanyasaji si tu upo kwa wanawake lakini hata kwa wanaume pia upo.

 

Akijibu swali katika kipindi cha mapito kinachorushwa ndani ya studio za Global Radio na Global TV Mwanaharakati anayepambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake ambaye pia ni mume wa mwanaharakati mwenzie Joyce Kiria, anayefahamika kwa jina la Aron amesema licha ya wanaume kunyanyaswa na wanawake lakini takwimu za unyanyasaji nyingi zinaonesha wanaume ndiyo wanyanyasaji wakubwa kuliko wanawake.

Mwanaharakati wa haki za wanawake Joyce Kiria

Ametolea mfano mwanamke tajiri na mwanaume tajiri akibainisha kwamba kuna wanaume ambao wanaishi na wanawake lakini hawafanyi kazi na wanalelewa vizuri tu bila manyanyaso lakini ukikuta mwanaume ambaye ni tajiri anaishi na mwanamke ambaye hana kazi mara nyingi wanaishia kunyanyasika.

 

Amesema jitihada kubwa inabidi zifanyike na elimu kubwa itolewe juu ya kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia hasa maeneo ya vijijini ambako wanawake wengi wananyanyasika na kuachiwa watoto ambao wanapambana nao katika malezi bila msaada wowote.

Leave A Reply