The House of Favourite Newspapers

Milioni kumi za Tigo Jigiftishe zaenda kwa muosha magari Tabata Dar

Mshindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja, Idrisa Selemani (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama.
Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja, Asha Shaban (wa pil kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama.
Mmoja wa washindi wa zawadi za kila siku, Anna Eliudi (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama.
Iyaka Seifu Muinga (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Bidhaa wa Tigo, Suleiman Bushangama (kulia).
Washindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo wakiwa katika picha ya pamoja.

 

KITITA cha shilingi milioni 10 cha mshindi wa kila wiki katika promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, kimenyakuliwa na Iyaka Seifu Muinga, anayefanya kazi ya kuosha magari maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam.

 

Muinga anakuwa ni mshindi wa pili wa zawadi ya shilingi milioni 10 baada ya milioni kumi ya kwanza kuchukuliwa na David John Mmuni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

 

Akipokea zawadi yake katika eneo analofanyia  kazi kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushangama, mshindi huyo alielezea furaha yake na kusema kuwa Tigo imemkomboa kwa kuwa amepata mtaji wa kufungua biashara.

 

‘Nimefurahi sana kuibuka na mtaji huu kutoka promosheni ya Jigiftishe. Nitatumia pesa hizi kufungua biashara, ila kusema kweli sina mpango wa kuacha kazi yangu ya sasa,” Iyaka alisema huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake waliomsindikiza jukwaani kupokea zawadi.

 

Akiongea  wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yahe, Bushangama aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu.

 

Pamoja na kukabidhi zawadi  ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa wiki, washindi wengine kumi wa kila siku kutoka mkoa wa Dar es Salaam walizawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja.

 

Promosheni hiyo ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

 

Jigiftishe inalenga kuongeza idadi ya mamilionea katika msimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi  moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni hiyo inayoendelea.

Comments are closed.