The House of Favourite Newspapers

Mimba kuchoropoka (Miscarriage)

0

1100_seven_most_common_miscarriage_causesTatizo la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi. Leo tutalijadili kwa kina tatizo hili ambalo kitaalamu huitwa Miscarriage.

MISCARRIAGE NI NINI?
Kwa kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.

Inapotokea kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.

Katika hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha kifo.
NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).

NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE?
Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.
Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)

Hitilafu katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki 13.

Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya mtoto na kusababisha Reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.

2. Upungufu wa homoni (Progesterone Deficiency)
Homoni ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo husababisha ujauzito kuharibika na kutoka kabla ya muda wake.

3. Umri mkubwa
Kwa kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli (Sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.

4. Magonjwa
Wanawake wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (Obesity), Polycystic Ovary Syndrome), malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.

5. Hitilafu katika kizazi
Baadhi ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (Uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.

6. Maambukizi ya bakteria au fangasi
Maambukizi ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo husababisha mimba kuchoropoka.

Sababu nyingine ni pamoja na matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):
1. Kutokwa na damu sehemu za siri
Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply