The House of Favourite Newspapers

MINAJ, HAMILTON WAJIVINJARI KIMAPENZI DUBAI

STAA mwanamitindo wa Marekani, Nicki Minaj na nyota mwendesha magari wa Formula One, Lewis Hamilton, wameibua sintofahamu kuhusu uhusiano wao ambapo wameonekana wakiwa pamoja huko Dubai baada ya picha zao kumwagika katika mtandao wa Instagram wakiendesha kigari maalum katika mchanga wa eneo hilo ambalo ni jangwa.

Wawili hao walionekana wamevaa kofia maalum za mashindano ya magari, na katika posti yake, Minaji aliandika kuhusu picha yake:

“Caribbean tingz what I on. Me & Lewis gettin paper like what ink dry on.”   Wakati Hamilton aliandika: “Riders” kwenye picha yake.

Nicki Minaj and Lewis Hamilton

Hamilton na Minaj mwanzo walionekana katika pati ya Tommy Hilfiger wakati wa maonyesho ya fasheni yaitwayo  New York Fashion Week ambapo tangu wakati huo wamekuwa wakionyesha hisia za ‘maelewano’ katika picha wanazotuma kwenye mtandao wa Instagram.

Nicki Minaj and Lewis Hamilton

Nicki ameongeza kusema kwamba uhusiano huo ni “mpya kidogo” na kwamba mshikaji wake huyo amekuwa akijivinjari naye kwa wiki kadhaa sasa.

“i love new boi,” amewahi kuandika Malkia huyo wa rapa katika posti moja kabla ya kuifuta.

Comments are closed.