The House of Favourite Newspapers

Mjane wa Gaddafi Akata Rufaa Nchini Malta Kupinga Mabilioni ya Pesa Kurudi Libya

0
Safiya Ferkash Mjane wa Hayati Muammar Gaddafi

MJANE wa aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muammar Gaddafi amekata rufaa ya maamuzi ya Mahakama ya nchini Malta iliyoidhinisha kiasi cha Euro milioni 95 zilizokuwa zimehifadhiwa katika Benki Kuu ya Nchi hiyo kurudishwa katika Serikali ya nchi ya Libya.

Mwanasheria kutoka nchini Malta, Louis Cassar Pullicino

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama Kuu ya nchi hiyo ni kwamba kiasi hichocha fedha kilihifadhiwa na aliyekuwa motto wa hayati Gaddafi, Mutassim Gaddafi ambaye naye aliuawa wakati wa vita ya kumuondoa madarakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.

 

Safiya Ferkash pamoja na mwanasheria wake wamesema Mahakama ya Malta haina ushahidi wa kutosha na hivyo hawana uwezo wa kuruhusu pesa hiyo irudi nchini Libya.

Aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muammar Gaddafi akiwa na mtoto wake ambaye naye ni marehemu, Mutassim Gaddafi

Hukumu ilitolewa mwezi Juni mwaka huu ikiwa ni baada ya kipindi cha miaka 10 cha mapambano ya kisheria.

 

Rufaa hiyo imekatwa kwa niaba ya mrithi wa Gaddafi na Mwanasheria kutoka nchini Malta, Louis Cassar Pullicino ingawa hadi sasa haijawekwa wazi ni lini rufaa hiyo itasikilizwa.

Leave A Reply