The House of Favourite Newspapers

Mkali wa Kagere Kumbe ni Sabato

REKODI bado zinaendelea kuandikwa kwenye ligi ya msimu huu ambapo baada ya Meddie Kagere kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao la mapema dakika ya pili kisha Mrisho Ngassa dakika ya kwanza mchezaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato amewafunika wote.

 

Sabato alifanya hivyo katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro baada ya kufunga bao la kwanza ndani ya sekunde 53. Akizungumza na Spoti Xtra, Sabato alisema; “Kila mchezaji nia yake ni kuona timu inafanikiwa kupata matokeo hivyo nitaendelea kufanya hivyo kila ninapopata nafasi kwenye timu yangu.”

“Ushindani ni mkubwa na ndio maana ukiangalia zimepita mechi nyingi mpaka kufanya hivyo nina imani kuna mengi ambayo yatatokea msimu huu kutokana na ushindani uliopo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Sabato.

 

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa bao la mapema la Sabato lilisaidia kuivuruga Ruvu Shooting ya Masau Bwire na kufanikisha kuongeza mengine matatu kwa kuwa wachezaji walipaniki.

LUNYAMADZO MLYUKA, SPOTI XTRA

Comments are closed.