The House of Favourite Newspapers

MKAZI WA BOKO DAR AKABIDHIWA GARI MPYA RENAULT KWID TOKA M-PESA


Mshindi wa  sita  wa gari  aina ya Renault Kwid  la promosheni ya  kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa, Batholomeo Kanjo mkazi wa Boko  jijini Dar es Salaam, akishuhudiwa na mke wake Frida Saimoni (kushoto) akikabidhiwa na Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Dar es Salaam, na Pwani, George Lugata  funguo za gari  wakati wa hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Mwenge jijini Dar es alaam. Yamebakia magari manne ili kushinda mteja wa Vodacom unatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa tu.
Batholomeo akizungumzia furaha yake baada ya kukabidhiwa gari.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Jacqueline Materu, akiongea kwa waandishi wa Habari pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Mwenge jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla kumkabidhi  Mshindi wa  sita  wa gari  aina ya Renault Kwid.
Balozi wa Miaka 10 ya M-Pesa,  Idrisa Sultan, akionge na wananchi waliojitokezwa kwenye  Viwanja vya Mwenge  wakati wa hafla ya kumkabidhi mshindi wa  sita  wa gari  aina ya Renault Kwid  la promosheni ya  kusherehekea miaka kumi ya M-Pesa. Yamebakia magari Manne ili kushinda mteja wa Vodacom unatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa tu kwa Kupiga *150*00#
Batholomeo Kanjo (watatu kushoto) akitoa ushuhuda njisi alivyoibuka mshindi  wa Promosheni ya M-Pesa  wakati wa hafla ya kumkabidhi gari  hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Mwenge jijini Dar es Salaam  huku akishuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Jacqueline Materu ( kushoto) Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, George Lugata, Balozi wa M-Pesa Idrisa Sultan, Mkuu wa Kitengo cha Mipango Mkakati na Ripoti wa Vodacom Tanzania, Nelusigwe Mwagota na  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa M-Pesa Happymark Mbeteni. 
Mkuu wa Vodacom Tanzania Plc, Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, George Lugata, (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 1  mkazi wa Mwenge Samweli Joseph baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya M-Pesa ,  wakati wa hafla kumkabidhi gari    aina ya Renault Kwid  mshindi wa sita Batholomeo Kanjo  iliyofanyika katika Viwanja vya Mwenge jijini Dar es alaam .  Wapili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango Mkakati na Ripoti wa Vodacom Tanzania, Nelusigwe Mwagota Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa M-Pesa Happymark Mbeteni.

 

 

Comments are closed.