The House of Favourite Newspapers

Mke Amnyoa Cannavaro Rasta

Beki wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’

MARA baada ya kuteuliwa kuwa Meneja Mpya wa Taifa Stars, beki wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, mke wake amemnyoa rasta.

 

Hali hiyo imetokea siku moja kabla timu ya Taifa haijaingia kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya Chan dhidi ya Kenya.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Cannavaro alisema hivi sasa ana muonekano mpya wa nywele zake baada ya mke wake kumwambia anyoe rasta alizokuwa nazo.

 

“Mimi siku zote ninaheshimu mawazo na ushauri wa mke wangu siku zote kama unavyoniona (anavua kofia na kuonyesha nywele zake) nimezinyoa rasta zangu nilizokuwa nazo kwa kipindi kirefu kabla ya kutangaza kustaafu kucheza soka.

“Baada ya kutangazwa kuwa meneja wa Stars mke wangu aliniambia nizinyoe kwa kuwa hazileti muonekano mzuri, kweli nikafanya hivyo na sasa niko hivi nilivyo,” alisema beki huyo wa zamani wa Taifa Stars.

Comments are closed.