Mke wa Afisa Mkuu Mtendaji wa OceanGate ni Kitukuu wa Abiria Wawili wa Titanic

Wendy Rush ni mke wa Stockton Rush, bosi wa OceanGate ambaye yuko kwenye nyambizi iliyotoweka baharibi ambayo inasakwa .
Yeye pia ni kitukuu wa Isidor na Ida Straus- abiria wawili waliokuwa kwenye meli ya Titanic ilipozama mwaka wa 1912.
Bi Rush, nee Hollings Weil, alifunga ndoa na Stockton Rush mnamo 1986, kulingana na tangazo la harusi yao katika New York Times..
Yeye ni mkurugenzi wa mawasiliano katika OceanGate na amekuwa katika safari tatu kwenye eneo la ajali ya Titanic, ukurasa wake wa LinkedIn unasema.

Strauses walikuwa miongoni mwa abiria tajiri zaidi wa Titanic.Isidor na kaka yake Nathan walikuwa wamiliki wa duka kuu la Macy.
Walionusurika walikumbuka kuona Isidor akikataa kiti kwenye mashua ya kuokoa maisha hadi wanawake na watoto wote walipopanda.Ida, mke wake wa miaka 40, alikataa kwenda bila mume wake.Wawili hao walionekana kukumbatiana huku meli ikizama.
Toleo la kubuniwa la tukio hili lilionyeshwa katika filamu ya 1997, ikionyesha wanandoa wakikumbatiana kitandani maji yanapoongezeka karibu nao.
Kulingana na kumbukumbu za New York Times, mwili wa Isidor ulipatikana baharini karibu wiki mbili baada ya kuzama.Mwili wa Ida hakupatikana.

