The House of Favourite Newspapers

MKE WA MUGABE ALIUNGA MKONO KUJIUZULU MUMEWE

GRACE MUGABE, mke wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ameripotiwa kwamba alimuunga mkono mumewe huyo katika hatua yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Kwa mujibu wa George Charamba aliyekuwa msemaji wa Mugabe, Grace ambaye alikuwa na nia ya kuwa rais wa nchi hiyo, anasemekana aliongoza kampeni ya kumwondoa aliyekuwa makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa.

 

Mwanamke huyo alikuwa ndiye kiongozi wa lililoitwa kundi la G40 ambalo hadi kufikia Novemba 15 mwaka jana, lilikuwa na nguvu kubwa katika chama tawala cha ZANU-PF. Grace alikuwa na uhakika wa kuwa mmoja wa makamu wawili wa rais baada ya kufukuzwa kwa Mnangagwa hapo Novemba 6 huku akiwa anaongoza kundi la upande mwingine katika mbio za kuwania urais.

 

Kwa mujibu wa Charamba, Grace ndiye aliyeshinikiza kujiuzulu kwa Mugabe baada ya jeshi kuingilia mnamo Novemba, liliandika gazeti la Daily News. “Hata mke wa rais alikuwa anashinikiza kujiuzulu kwa Mugabe,” amenukuliwa Charamba akisema na kuongeza kwamba kabla ya hapo Mugabe alikuwa anataka aachie madaraka kwa wakati aliokuwa akitaka yeye, lakini mambo yalikuwa yameanza kuwa magumu kwani watu waliokuwa wanamuunga mkono walikuwa wameamua kuachana naye.

Inasemakana Charamba alimwambia kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kwamba nafasi yake ilikuwa hatarini, ikiwa ni pamoja na maandamano ya makumi ya maelfu ya Wazimbabwe waliofurika mitaani mwa jiji la Harare kuliunga mkono jeshi.

 

“Nilimwambia shefu (kiongozi kwa lugha ya Zimbabwe ya Kishona) unatazama upande mmoja tu; kuna upande mwingine ambao utakuletea madhara,” anasema Charamba. Hatimaye Mugabe aliachia madaraka Novemba 21 na kujiokoa kushitakiwa huku akiacha shangwe mitaani usiku kucha kutokana na kujiuzulu huko. Hata hivyo, Mugabe amehakikishiwa na serikali ya Mnangagwa marupurupu mazuri na usalama wake.

 

BREAKING NEWS: Aliyewauwa Mtoto na Mkewe kwa Jembe Akamatwa Iringa

Comments are closed.