MKE WA TRUMP JR AUGUA GHAFLA KWA KUFUNGUA BARUA YENYE UNGA

Mke wa Donald Trump Jr, Vanessa amekimbizwa katika Hospitali ya Manhattan muda mfupi uliopita baada ya kufungua barua ambayo ndani yake kulikuwa na vitu kama unga mweupe.

Inasemekana barua hiyo ilikuwa imetumwa kwa mume wake ambaye ni mtoto wa kwanza wa Rais Donald Trump aliyezaa na mkewe wa zamani Ivana, Donald Trump Jr

Inasemekana baada tu ya kuifungua barua hiyo, watu watatu wa nyumba hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya New York Presbyterian-Weill Cornell Medical Center kwa ajili ya matibabu kutokana na afya zao kubadilika ghafla.

Aidha, baada ya sampuli ya unga kupelekwa maabara kwa ajili ya vipimo, imebainika kuwa unga huo hauna sumu wala madhara yoyote japo uchunguzi zaidi unaendelea kubaini tatizo na iwapo unga huo una madhara kwa binadamu.

Toa comment