The House of Favourite Newspapers

Mkono wa Fundi Seremala Uliokatwa Waunganishwa – Pichaz

FUNDI seremala ambaye mkono wake ulibaki ukining’inia kati ya ngozi na mfupa baada ya kupata ajali mbaya ya kukatwa na msumeno wa umeme, amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa kuungwa mkono huo. Anthony Lelliott, mwenye umri wa miaka 46, mkono wake wa kushoto ulikuwa karibu kukatika wote katika sehemu mbili wakati alipokuwa anakata bodi ya sakafu kwa mashine yenye nguvu.

 

Alifanyiwa upasuaji kwa muda wa saa 17 katika hospitali ya Mt.George huko kusini mwa London, Uingereza. Madaktari waliomtibu wanasema kuwa tatizo lake lilikuwa kubwa ambalo hawajawahi kukutana nalo. Mtaalam wa upasuaji wa plastiki, Roger Adlard, alifanya operesheni ya awali kwa saa 13 akishirikiana na mwenzake, Farida Ali.

Adlard alisema: “Kuna wataalamu wengi wa upasuaji ambao wangeona ukubwa wa jeraha, wangefikiria kuwa asingepona. Lelliott alikatwa na meno ya msumeno huo, hivyoa halikuwa jeraha lililonyooka.” Mkono wa Lelliott ulikuwa bado umeshikana lakini kwa ngozi tu na mfupa mdogo. Alipoteza damu nyingi na hakuwa na kumbukumbu ya ajali iliyompata.
“Nilijua kuwa upasuaji huu utachukua muda mrefu,” mtaalamu wa upasuaji alieleza.

 

Katika upasuaji wa kwanza, timu ya upasuaji walifanya kazi usiku mzima kuhakikisha kuwa kuna msukumo mzuri wa damu na mishipa inapeleka damu katika vidole vingi iwezekanavyo. Baada ya kuunga mfupa uliokuwa umeharibika, walitoa mishipa ya miguu.

 

Umakini mkubwa ulikuwa unahitajika kwa ajili ya kuunga kila kitu. Madaktari wanasema kuwa waligundua kuwa sehemu ya ngozi ya Lelliott ilikuwa imepata maambukizi ya vimelea na kidole chake cha katikati kiliharibika vibaya sana hivyo kisingeweza kupona.

“Tumefanya maamuzi ya kuona namna ya kuokoa mkono wote, inabidi kidole cha katikati kiondoke ili kisaidie kuweka ngozi kuwa sawa na mfupa uliotoka katika mkono. Tatizo lingine lilikuwa ni kupata ngozi ya kutosha kufunika eneo hilo. Mkono wake hauwezi kurudi katika hali yake ya kawaida, lakini tuna matumaini kuwa kuna namna ya ufanyaji kazi wake utarudi kuwa kama awali lakini anaweza kukunja mkono na kushika hata kalamu na kuandika.”

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza (BBC), Lelliott amefurahia huduma nzuri aliyoipata na anasema:  “Ninamshukuru kila mmoja aliyenihudumia, kwa sababu nilikuwa nafikiri nitakuwa ninaamka bila kuwa na mkono wangu mmoja. Kwa sasa ninajaribu tu kuzoea namna ya kuutumia, ninashukuru sana”.

Comments are closed.