Mkuu wa Mkoa Dar atembelea Maonyesho ya Wajasiriamali Mnazimmoja
Mkuu wa Mkoa, Sadick Mecky Said (kushoto) akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar kutembelea maadhimisho ya wajasiriamali.…Akisaini kwenye kitabu cha wageni kilichokuwa kwenye banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki.…Akipewa maelekezo.Vijana waliokuwa kwenye banda la Tanzania wakimpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Sadick Mecky Said akisaini kwenye kitabu cha wageni ndani ya banda la Burundi.Banda la Uganda kwenye maonesho hayo.Mabanda maalumu yaliyokuwemo kwenye maonesho hayo.Mkuu wa Mkoa akisalimia akina mama waliokuwa kwenye maonesho hayo.Bidhaa mbalimbali kwenye maonesho hayo.Banda la Burundi linavyoonekana.Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.Brass Band ya polisi ikijiandaa kutoa burudani.Sadick Mecky Said akitembelea mabanda mengine kwenye maonesho hayo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said, leo ametembelea maonyesho ya 16 ya wajasiriamali wa sekta zisizo rasmi wa Afrika Mashariki.
Maonyesho hayo yalianza Novemba 30, mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar, yakitarajiwa kumalizika Desemba 6, ambapo yamekutanisha nchi za Afrika Masharika za Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda.
Watu mbalimbali wameyatembelea mabanda yaliyomo ndani ya viwanja hivyo na kujionea huduma mbalimbali zinazofanywa ambapo kaulimbiu yake ni: “Nunua bidhaa za Afrika Mashariki ujenge uchumi wa Afrika Mashariki’’.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments are closed.