The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Mkoa Dar atembelea Maonyesho ya Wajasiriamali  Mnazimmoja

1.Mkuu wa Mkoa,Sadick Mecky Said (kushoto) akiwasili katika viwanja vya mnazi mmoja Dar kutembelea maadhimisho ya wajasiliamali.Mkuu wa Mkoa, Sadick Mecky Said (kushoto) akiwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar kutembelea maadhimisho ya wajasiriamali.2.Mkuu wa Mkoa,Sadick Mecky Said akisaini kwenye kitabu cha wageni kilichokuwa kwenye banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki.…Akisaini kwenye kitabu cha wageni kilichokuwa kwenye banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki.3.Akipewa maelekezo kwenye banda hilo la Jumuiya ya Afrika Mashariki.…Akipewa maelekezo.4.Vijana waliokuwa kwenye banda la hapa nchini wakimpa maelekezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, juu ya huduma wanazozitoa.Vijana waliokuwa kwenye banda la  Tanzania wakimpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.5.Sadick Mecky Said akisaini kwenye kitabu cha wageni ndani ya banda maalum la nchi ya Burundi lililokuwa kwenye maadhimisho hayo.Sadick Mecky Said akisaini kwenye kitabu cha wageni ndani ya banda la Burundi.6.Banda la nchini Uganda likionekana kwenye maonesho hayo.Banda la Uganda kwenye maonesho hayo.7.Mabanda maalumu yaliyokuwemo kwenye maonesho hayo yanayowakilisha nchi, za Afrika Mashariki.Mabanda maalumu yaliyokuwemo kwenye maonesho hayo.8.Mkuu wa Mkoa akisalimia akina mama waliokuwa kwenye maonesho ya bidhaa mbalimbali viwanja vya mnazi mmoja.Mkuu wa Mkoa akisalimia akina mama waliokuwa kwenye maonesho hayo.9.Bidhaa mbalimbali zilizokuwemo kwenye maonesho hayo.Bidhaa mbalimbali kwenye maonesho hayo.10.Banda la maonesho ya bidhaa za nchini Burundi kama linavyoonekana.Banda la Burundi linavyoonekana.11.Kikundi cha ngoma kikitoa burudani kwenye maonesho hayo.Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.12.Blasbandi ya polisi ikijiandaa kutoa burudani.Brass Band ya polisi ikijiandaa kutoa burudani.13...mkuu wa mkoa akizidi kutembezwa kwenye mabanda mbalimbali yaliyokuwa kwenye maonesho hayo.Sadick Mecky Said akitembelea mabanda mengine kwenye maonesho hayo.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said, leo ametembelea maonyesho  ya 16 ya wajasiriamali wa sekta zisizo rasmi wa Afrika Mashariki.

Maonyesho hayo yalianza Novemba 30, mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar,  yakitarajiwa kumalizika Desemba 6,  ambapo yamekutanisha nchi  za Afrika Masharika za Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda.

Watu mbalimbali wameyatembelea mabanda yaliyomo ndani ya viwanja hivyo na kujionea huduma mbalimbali zinazofanywa ambapo kaulimbiu yake  ni:  “Nunua bidhaa za Afrika Mashariki ujenge uchumi wa Afrika Mashariki’’.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.