MKUU WA SHULE MWENYEHERI ANUARITE ATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS
MKUU wa Shule ya Sekondari ya Mwenyeheri Anuarite iliyopo Kimara jijini Dar es Salaam, Carlos Mgumba hivi karibuni alitembelea ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.
Akiwa ofisini hapo, alisema amefurahi kujionea kazi zinazofanywa ambapo alifarijika kuona kampuni hiyo ikiwa na vijana wengi wakifanya kazi hapo ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa la kesho.
Mgumba aliweza kutembelea idara mbalimbali za magazeti Pendwa ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi na gazeti la Michezo la Championi na kubadilishana mawazo na wahariri pamoja na waandishi wa magazeti hayo ikiwa ni moja ya kukuza mahusiano mema.
Aidha katika matembezi yake aliambatana na mwanafunzi wake ambaye ni mhitimu wa kidato cha sita, Prosper Nyambe ambaye aliweza kufanya mahojiano kupitia Global TV Online juu ya kipaji chake alichonacho.
Mkuu huyo alisema shule yake inawapatia wanafunzi wake elimu ya ziada ya kuelewa namna ambavyo wanaweza kujikwamua kiuchumi wamalizapo masomo yao kupitia midahalo mbalimbali ambazo zimepelekea kuibua kipaji cha mwanafunzi huyo.
Na Denis Mtima/GPL
Comments are closed.