The House of Favourite Newspapers

Mlinga: ‘Maprofesa wa Tanzania Wana Matatizo Gani’?

 

MBUNGE wa Ulanga mkoani Morogoro, Goodluck Mlinga (CCM) amemvaa Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekonolojia, Prof. Joyce Ndalichako akidai kuwa waziri huyo ameshindwa kusimamia vyema wizara yake na kusababisha shule nyingi za serikali kushindwa kufaulisha vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni na NECTA.

 

Akichangia mjadala Bungeni mjini Dodoma jana kuhusu wizara ya elimu, Mulinga aisema;

 

“Kwa muda wa miaka miwili sasa tumeshuhudia uangukaji mkubwa katika matokeo ya mitihani kwa shule za serikali hapa nchini, kwa hili waziri anaweza kujipima mwenyewe… Mimi sijui maprofesa wa Tanzania wana matatizo gani? Ningekuwa Rais, ningemchagua mtu kama Msukuma (Mbunge wa Geita) au Lusinde ambao wameishia darasa la saba kwa kuwa wanafahamu mataizo katika sekta ya elimu ambayo yaliwafanya wakashindwa kuendelea na elimu zaidi.

 

“Tulizoea kuona shule za serikali zikiongoza, leo hii katika 100 bora kuna shule za serikali nne tu, zingine ni za binafsi. Lakini cha kushangaza waziri anapiga vita shule za binafsi, hivi hizi shule zisingekuwepo, Prof. Ndalichako leo si ungekuwa waziri wa masifuri tu?

 

“Walimu mnawapangia maeneo ya vijijini,hakuna nyumba, wanaishi kama makomandoo. Walimu wanafanya kazi mpaka wikiendi lakini hawapati posho, huu ni uonevu,” alisema Mlinga.

 

VIDEO: MSIKIE MLINGA AKIFUNGUKA

Comments are closed.