Mmiliki wa mabasi ya Sauli Apata Ajali ya Gari, Afariki Dunia – Video

Mmiliki wa mabasi ya Sauli yanayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Mbeya, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi mkoa Pwani Pius Lutumo amesema ajali hiyo ilihusisha magari mawili yaliyokuwa katika sehemu moja gari namba T213 DQD aina ya Fuso.
Ameeleza kuwa gari hilo lilipata hitilafu ya kiufundi na kuligonga gari aina ya Jeep lenye namba za usajili T 466 EGW alilokuwemo mmiliki wa mabasi ya Sauli ambapo nalo liligonga gari jingine aina ya Howo la kubebea kokoto.
Wakati marehemu anapata ajali hiyo alikuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka minne ambaye alipata michubuko na alipelekwa hospitali kabla ya kuruhusiwa.

